Mtunzi: Cpa M. B. Ngooh
> Mfahamu Zaidi Cpa M. B. Ngooh
> Tazama Nyimbo nyingine za Cpa M. B. Ngooh
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: Melkior Ngooh
Umepakuliwa mara 332 | Umetazamwa mara 1,464
Download Nota Download Midi
Kiitikio:
Tuamke sasa (twendeni kwa Bwana) tukamtolee dhabihu, dhabihu za kumshukuru, tumrudishie (Bwana) kwani vyote tulivyo navyo ni mali yake, (kumtolea Mungu) ni kutengeneza njia ya wokovu, wokovu wa Milele X2
Mashairi:
Tutoe kwa moyo, asema Bwana, nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, kama sina upendo mimi, haisaidii kitu.
Tutoe bila manung’uniko, asema Bwana, nikitoa mwili wangu wote, mwili wangu niungue moto, kama sina upendo mimi, haisaidii kitu.
Ikiwa una neno na ndugu yako, kapatane nae ndipo urudi utoe sadaka yako, hapo ndipo sadaka yako itampendeza Mungu.