Mtunzi: Cpa M. B. Ngooh
> Mfahamu Zaidi Cpa M. B. Ngooh
> Tazama Nyimbo nyingine za Cpa M. B. Ngooh
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: Melkior Ngooh
Umepakuliwa mara 634 | Umetazamwa mara 2,274
Download Nota Download MidiKiitikio:
Sadaka
yangu ikupendeze ee Bwana kama sadaka ile ya (mwanamke) mjane maskini ilivyokupendeza,
maana wengineo walitoa baadhi ya mali zao lakini (mwanamke) mjane katika
umaskini wake alitoa vyote alivyokuwa navyo. Alitoa kwa moyo (mwanamke) mjane
katika umaskini wake alitoa vyote alivyokuwa navyo.
Mashairi:
1.
Mwanamke
mjane na maskini alitoa senti mbili, alitoa vyote kwa upendo na ukarimu.
2.
Tusijiwekee
hazina duniani, tuwekeze Mbinguni ambako nondo wala wevi hawaharibu.
3.
Hazina
yako ilipo ndipo moyo wako ulipo, tumtolee Mungu sadaka kwa ukarimu.