Ingia / Jisajili

Emmanueli Leo Kazaliwa

Mtunzi: Respice Makoko
> Mfahamu Zaidi Respice Makoko
> Tazama Nyimbo nyingine za Respice Makoko

Makundi Nyimbo: Noeli

Umepakiwa na: RESPICE MAKOKO

Umepakuliwa mara 1,741 | Umetazamwa mara 4,769

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

EMMANUELI LEO KAZALIWA

KIITIKIO

Emmanueli leo kazaliwa Bethlehemu amezaliwa kwa ajili yetu sisi.x2

Tumshangilie (sote) tupige na makofi na vigelegele kwa shangwe kubwa.x2

MASHAIRI

  1. Leo Bethlehemu mtoto kazaliwa amezaliwa kwa ajili yetu sisi tumpokee kwa furaha na vifijo.
  2. Amelazwa ndani ya hori la wanyama ni mto-to mpole mtulivu kasinzia twende tumsalimu leo katujia.
  3. Leo tumepata mwangaza duniani utuangaze ndani ya mioyo yetu utuongoze ili tufike mbinguni.
  4. Malaika wanafurahi huko juu wafurahia kuzaliwa kwa masiya na wanaimba nyimbo nzuri kwa furaha.
  5. Utukufu kwa Mungu Baba juu mbinguni nayo amani iwe duniani pote na kwa watu wote wenye mapenzi mema.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa