Ingia / Jisajili

Hodi Hodi Ninabisha (Ngo! Ngo! Ngo!)

Mtunzi: Elijah M Kilonzi
> Mfahamu Zaidi Elijah M Kilonzi
> Tazama Nyimbo nyingine za Elijah M Kilonzi

Makundi Nyimbo: Mwanzo

Umepakiwa na: ELIJAH Mulei

Umepakuliwa mara 172 | Umetazamwa mara 316

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Hodi hodi ninabisha-ninabisha nyumbani mwako, Bwana Mungu unifungulie-niingie nyumbani mwako; Ninabisha hodi(ngo ngo ngo) unifungulie; njooni wote tumwabudu Bwana.x2 1. Wakusanyikao kwa ajili yangu- Bwana asema yu kati yao; Kwa kukusanyika leo natujue- Bwana Mungu yu kati yetu. 2. Umenitendea mema mengi kweli - Wema wako hauna mwisho; Kwa mema ambayo umenitendea – Naja Bwana nikushukuru. 3. Njooni kwangu wale mmelemewa - Na mizigo niwapumzishe; Mzigo wa dhambi kanichosha mimi- Naja Bwana nipumzishe. 4. Naileta sala yangu kwako Bwana - Nakusihi isikilize Na sadaka yangu ee Bwana naleta – ibariki ifae kwako

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa