Mtunzi: Br. Stan Mkombo, Ofmcap
> Tazama Nyimbo nyingine za Br. Stan Mkombo, Ofmcap
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Kristu Mfalme | Mafundisho / Tafakari | Matawi | Zaburi
Umepakiwa na: Stanslaus Mkombo
Umepakuliwa mara 957 | Umetazamwa mara 3,377
Download Nota Download MidiINUKA EE BWANA [Br. Stanslaus Mkombo, OFMCap.]
[Zaburi ya Maandamano, Taz. Hes 10:35; Zab. 68:1-3 & Zab 24: 7-10]
// Inuka ee Bwana, adui zako watawanyike, na hao wakuchukiao wakimbie mbele zako.//x2
1. Kama moshi upeperushwavyo, ndivyo uwapeperushavyo wao; Kama nta motoni waovu hutoweka mbele zako.
2. Bali wenye haki hufurahi, huushangilia uso wa Mungu; hupiga kelele kwa furaha kumshukuru Mungu wao.
3. Inukeni enyi malango, enyi malango ya milele; Bwana na Mfalme wa Utukufu apate kuingia.
4. Nani Mfalme wa Utukufu? Bwana mwenye nguvu, hodari; Bwana mungu wa majeshi hodari hodari wa vita.