Mtunzi: Br. Stan Mkombo, Ofmcap
> Tazama Nyimbo nyingine za Br. Stan Mkombo, Ofmcap
Makundi Nyimbo: Majilio | Matawi | Zaburi
Umepakiwa na: Stanslaus Mkombo
Umepakuliwa mara 560 | Umetazamwa mara 2,607
Download Nota Download MidiINUKENI ENYI MALANGO [Br. Stanslaus Mkombo, OFMCap.]
//(III: Inukeni enyi malango), (wote) Inukeni enyi enyi malango ya milele, Mfalme Mtukufu apate kuingia, Yeye Bwana ni Mfalme wa Utukufu.//X2
//(I&II: Inukeni ee malango) (wote) Ya milele, (I&II Bwana Mfale Mtukufu) (wote) Apate kuingia.//x2
Mashairi
1. Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana,/ dunia na wote wakaao ndani yake; /Maana kaiweka misingi yake juu ya bahari,/ na juu ya mito ya maji /aliithibitisha
2. Ni nani atakayepanda mlima wa Bwana/ na kusimama patakatifu pake Bwana?/ Ni mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe;/ asiye iinua nafsi/ yake kwaubatili.
3. Atapokea atapokea baraka kwa Bwana/ na haki kwa Mungu, Mungu wa wokovu wake./ Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao e-e Mungu;/ watafutao uso wako/ ee Mungu wa Yakobo.
4. Inukeni inukeni ee malango ya milele, Mfalme Mtukufu apate kuingia. Ni nani Mfalme Mtukufu, Ni Bwana wa Majeshi; Bwana mwenye nguvu hodari, hodari wa vita.