Mtunzi: Br. Stan Mkombo, Ofmcap
> Tazama Nyimbo nyingine za Br. Stan Mkombo, Ofmcap
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Miito | Mwaka wa Familia (2014) | Ndoa | Shukrani | Zaburi
Umepakiwa na: Stanslaus Mkombo
Umepakuliwa mara 862 | Umetazamwa mara 2,806
Download Nota Download MidiNIREHEMIWE KUONA UZEE PAMOJA NAYE [Br. Stanslaus Mkombo, OFMCap]
[Wimbo wa Shukrani ya Ndoa kutokana na Tobiti 8:5-18]
Ee Mungu wa Baba zetu umehimidiwa, na Jina lako takatifu tukufu limehimidiwa milele.x2 Ndiwe uliyemwumba Adamu, ukampa Hawa, awe mke wake awe msaidizi tena awe tegemeo lake.
Nami kwa wema wako leo hii, umenipa ……[jina la Bi-arusi au “huyu”], awe mke wangu, awe msaidizi, tena awe tegemeo langu.
// (I,III&IV): Na sasa Bwana ninaomba huruma yako kwa kuwa
(Wote) Simtwai (IV: mke) mke wangu huyu kwa tama, bali katika kweli; Amuru nirehemiwe kuona uzee pamoja naye.//x2
Mashairi
1: Ee Bwana umehimidiwa, kwani umenifurahisha, umetutendea kadiri ya rehema zako nyingi.
2. Ee Bwana uwarehemu watoto wako hawa wawili, wamalize maisha katika afya, furaha na heri.