Ingia / Jisajili

Yu Heri Towashi

Mtunzi: Br. Stan Mkombo, Ofmcap
> Tazama Nyimbo nyingine za Br. Stan Mkombo, Ofmcap

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Miito | Watakatifu

Umepakiwa na: Stanslaus Mkombo

Umepakuliwa mara 521 | Umetazamwa mara 2,567

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

YU HERI TOWASHI

[Br. Stan Mkombo, OFMCap.]

//Yu heri towashi ambaye hakutenda yasiyo haki, wala kuwaza mambo maovu juu ya Bwana.

Naye Heri mwanamke asiyezaa maadamu yu safi, hakutaka kuchukua mimba kwa kukosa.// x2

1.       Yeye atakuwa na matunda wakati ule Bwana ata’pokuja kuziangalia roho za watumishi wake: (I-IV) Atapewa taji tukufu ya uzima milele.

2.       Yeye atapewa upendeleo na Bwana kwa uaminifu wake, kura yake katika ka patakatifu pa Bwana, (I-IV) itapendeza kuliko mke, wana na mabinti.

3.       Basi sasa matowashi wasiseme kwamba, ‘Mimi ni mti mkavu’, kwa maana Bwana awaambia matowashi: (I-IV) “Nitawapa nyumbani mwangu jina kuu milele.”


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa