Ingia / Jisajili

Njoo Atakurehemu

Mtunzi: Br. Stan Mkombo, Ofmcap
> Tazama Nyimbo nyingine za Br. Stan Mkombo, Ofmcap

Makundi Nyimbo: Kwaresma | Mwaka wa Huruma ya Mungu | Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Stanslaus Mkombo

Umepakuliwa mara 321 | Umetazamwa mara 1,650

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

NJOO ATAKUREHEMU [Br. Stanslaus Mkombo, OFMcap.]

1. Ewe Mkristu jongea kiti cha rehema cha Mungu, Yeye ni mwingi wa fadhili na rehema, na neema.

Chorus

//Njoo (kwake), Njoo (njoo), Njoo (kwake), Naye atakurehemu.//x2

2. Hakuna dhambi inayozidi huruma ya Mungu, dhambi zote atazitakasa kwa damu ya Yesu.

3. Dhambi zako zote zijapokuwa nyekundu sana, ataziosha na utakuwa mweupe kama sufu.

4. Ujapoishi kizuizini kwa muda mrefu, usiziogope changamoto za kukiondoa.

5.  Chukua hatua na Yeye atakusaidia, ujapokuwa dhaifu sana atakuwezesha.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa