Mtunzi: Br. Stan Mkombo, Ofmcap
> Tazama Nyimbo nyingine za Br. Stan Mkombo, Ofmcap
Makundi Nyimbo: Watakatifu | Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Stanslaus Mkombo
Umepakuliwa mara 853 | Umetazamwa mara 2,753
Download Nota Download Midi(I:Hawa ndio mashujaa wake Bwana) Hawa ndio mashujaa wake Bwana:
Walibatizwa ubatizo wa Bwana wao, wakapanda Kanisa kwa damu yao.
Waliukabili vema mslaba wao wakamaliza kazi na wakashinda;
[(I&II: Walikinywea kikombe chake Bwana) Hata wakawa marafiki wake Mungu. ]x2
1. Ndugu zetu wameshinda kwa damu ya mwanakondoo, na kwa nguvu ya ukweli ule walioutangaza; hawakuyathamini maisha yao kuwa kitu sana: (I&III) Kwa ajili ya Jina la Bwana walikuwa tayari kufa x2
2. Machoni pa watu wajinga walionekana wamekufa, na kufariki kwao kulidhaniwa kuwa ni hasara yao; Lakini wako mbele ya kiti cha enzi chake Mungu: (I&III) Nao wamtumikia Bwana mchana hata usiku x2
3. Naye Mungu atafanya makao yake katia yao, watakuwa watu wake naye atakuwa Mungu wao; Naye atayafuta machozi katika macho yao: (I&III) Ndipo hakutakuwa na kifo maumivu wala kilio x2
4. Watatawala pamoja naye, na kung’aa kama nyota mbinguni, kwani mungu kawajaribu na kuwaona wamestahili. Kama dhahabu katika tanuru aliwajabu: (I&III) Kisha Bwana akawakubali kwa mfano wa kafara x2