Mtunzi: Br. Stan Mkombo, Ofmcap
> Tazama Nyimbo nyingine za Br. Stan Mkombo, Ofmcap
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Miito | Shukrani
Umepakiwa na: Stanslaus Mkombo
Umepakuliwa mara 640 | Umetazamwa mara 2,484
Download Nota Download MidiKATIKA VYOMBO VYA UDONGO [Br. Stan Mkombo, OFMCap.]
1. Tumebeba hazina takatifu ya Mungu katika vyombo vya udongo; vyombo ni nafsi zetu zilizo dhaifu x2
Chorus
Sifa, utukufu milele viwe kwa Mungu Baba, na kwa Mwana, na Roho Mtakatifu.
Ndiye aliyetuwezesha kufika hata hapa; asifiwe, ahimidiwe milele.
2. Ili idhihirike wazi kuwa uwezo unaotenda kazi yake ndani mwetu si wetu, bali ni wa Mungu. x2
3. Tunasema asante Mama Maria, Fransisko na Watakatifu wote, nanyi wapendwa kwa sala na misaada. x2
[Baada ya Chorus ya mwisho malizia kwa kuimba Coda maneno yafuatayo]
Asante Baba, asante Mwana, Asante Roho Mtakatifu. x2