Ingia / Jisajili

Sasa Bwana - Wimbo Wa Simeoni

Mtunzi: Br. Stan Mkombo, Ofmcap
> Tazama Nyimbo nyingine za Br. Stan Mkombo, Ofmcap

Makundi Nyimbo: Shukrani | Watakatifu | Zaburi

Umepakiwa na: Stanslaus Mkombo

Umepakuliwa mara 1,429 | Umetazamwa mara 4,357

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

SASA BWANA - WIMBO WA SIMEONI [Br. Stanslaus Mkombo, OFMCap.]

//Sasa ee Bwana umetimiza ahadi yako, sasa waweza kuruhusu mtumishi wako, apumzike kwa amani.x2//

1. Kwa kuwa macho yangu, yameutazama, wokovu ulio ufunua ee Bwana, machoni pa mataifa yote.

2. Nuru ya kuwa Mwanga, wa mataifa yote, na kuwa utukufu wa watu wako, Taifa lako la Israeli.

3. Atukuzwe Baba, Mwana, na Yeye Roho Mtakatifu, kama mwanzo, na sasa, na siku zote, milele. Amina.


Maoni - Toa Maoni

Pius paschal Jul 28, 2022
Pongeza

Toa Maoni yako hapa