Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 654 | Umetazamwa mara 2,702
Download Nota Download MidiKwa unyenyekevu twende sote, yeye (Bwana Yesu) ametualika (sote) tule mwili wake tunywe damu yake tupate uzima (huo wa) milele
1.Ni karamu ya upatanisho,
atualika twende sote – twende ndugu twende
Karamuye yaleta amani,
tuishi kwa upendo wake – twende ndugu twende
2.Ndugu ujitayarishe kweli,
kumpokea Yesu Mwokozi –
Tule mwili tunywe damu pia,
kwa ukumbusho wake Kristu –
3.Bwana kwa upendo wake mkuu,
mema ya mbingu ametupa –
Tumejazwa na neema zake,
baraka za mbingu twapata –
4.Heri wale waulao mwili,
na kuinywa damu ya Yesu –
Chakula hiki ni cha uzima,
tukila twaishi milele –