Mtunzi: Br. Stan Mkombo, Ofmcap
> Tazama Nyimbo nyingine za Br. Stan Mkombo, Ofmcap
Makundi Nyimbo: Shukrani | Zaburi
Umepakiwa na: Stanslaus Mkombo
Umepakuliwa mara 1,907 | Umetazamwa mara 6,556
Download Nota Download MidiNI NENO JEMA KUMSHUKURU BWANA (Zab 92)
[Nd. Stanslaus L. Mkombo, OFMCap]
// Ni neno je---ma kumshukuru Bwana, (Mungu wetu) na kuliimbia Jina lako ee Uliye Juu, kuzitangaza rehema zako asubuhi, na uaminifu wako wakati wa usiku.//x2
1. I: Kwa chombo chenye nyuzi kumi, kwa kinanda na kwa mlio wa sauti tamu ya kinu-bi; (I-IV) Umenifurahisha Bwana, kwa kazi ya mikono yako; na kwa matendo yako nitashangilia.
2. II: Wasio haki wataangamizwa milele, maana hao adui zako Bwana watapotea;
(I-IV) Watendao maovu watatawanyika wote pia.
3. III: Lakini mwenye haki atasitawi kama mtende, atakuwa kama mwerezi wa Lebanoni; (I-IV) Waliopandwa nyumbani mwa Bwana watasitawi katika nyua zake.
4. IV: Watazaa matunda hata wakati wa uzee, watajaa utomvu watakuwa nao ubichi; watangaze ya kuwa Bwana ni mwenye adili, (I-IV) Ndani yake Mwamba wangu hamna udhalimu.