Ingia / Jisajili

Matunda ya Roho Mtakatifu

Mtunzi: Cpa M. B. Ngooh
> Mfahamu Zaidi Cpa M. B. Ngooh
> Tazama Nyimbo nyingine za Cpa M. B. Ngooh

Makundi Nyimbo: Pentekoste

Umepakiwa na: Melkior Ngooh

Umepakuliwa mara 485 | Umetazamwa mara 2,280

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio:

 

Ewe Roho Mtakatifu, nafsi ya tatu ya utatu Mtakatifu Mungu mmoja tunainua mikono yetu juu kupokea baraka zako, Roho Mtakatifu karibu uishi mioyoni mwetu X2

 

Mashairi:

 

  1. Washa mapendo ndani ya mioyo yetu, uwashe moto wa mapendo.

 

  1. Daima utujalie msingi wa amani, amani itawale kwetu.

 

  1. Tufanye kuwa chanzo cha furaha katika maisha, tueneze furaha kwa watu wote.

 

  1. Tujalie moyo wa uvumilivu, tuvumiliane na wenzetu.

 

  1. Tuchukuliane kwa wepesi na utu wema, tusameheane tunapokoseana.

 

  1. Tujalie fadhili za kumjua Mungu, tumjue Mungu na kumtumikia.

 

  1. Utujalie moyo wa upole, tuchukuliane kwa wema bila shari.

 

  1. Tujalie kiasi kwa mambo yanayomgusa Mungu, tusimkosee Mungu tushike amri zake.

 

  1. Utusaidie kuwa waadilifu, katika mambo yote ya roho na ya mwili.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa