Ingia / Jisajili

Yesu Amefufuka

Mtunzi: Cpa M. B. Ngooh
> Mfahamu Zaidi Cpa M. B. Ngooh
> Tazama Nyimbo nyingine za Cpa M. B. Ngooh

Makundi Nyimbo: Pasaka

Umepakiwa na: Melkior Ngooh

Umepakuliwa mara 104 | Umetazamwa mara 666

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Mwanzo Mkesha wa Pasaka
- Mwanzo Dominika ya Pasaka
- Antifona / Komunio Dominika ya 4 Mwaka B
- Antifona / Komunio Dominika ya 4 ya Pasaka Mwaka B

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio

 

Yesu ameshinda ameshinda mauti, yeye ndiye alpha na omega, ni mwanga na uzima wa milele. Tukimkiri Yesu kinywani mwetu ya kuwa yeye ni Bwana na kuamini mioyoni mwetu kuwa Mungu alimfufua kutoka wafu nasi tutakombolewa kutoka dhambini X2

 

Mashairi

 

  1. Ukuu na ufufuko wa Kristu ni uhakika wa wokovu wetu, tumshangilie na kufurahiwa nae na kufurahiwa nae.

 

  1. Kristu ndiye ufufuo na uzima wetu, tukimsadiki hatutakufa bali tutaishi tutakuwa na uzima wa milele tutaishi milele.

 

  1. Tukimkiri Yesu kwa kinywa chetu ya kuwa ni Mwokozi wetu na kuamini mioyoni mwetu tutakombolewa.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa