Mtunzi: Cpa M. B. Ngooh
> Mfahamu Zaidi Cpa M. B. Ngooh
> Tazama Nyimbo nyingine za Cpa M. B. Ngooh
Makundi Nyimbo: Watakatifu
Umepakiwa na: Melkior Ngooh
Umepakuliwa mara 281 | Umetazamwa mara 1,586
Download Nota Download Midi
Kiitikio
Ee mama Tereza (Mtetezi wa Wanyonge) tuombee tuige mfano wa maisha yako tuwapende na kuwajali masikini na fukara siku zote za maisha yetu kama njia ya kufikia wokovu wetu.
Mashairi
Ulisema hatuwezi kufanya mambo makubwa, lakini tunaweza kufanya mambo madogo kwa upendo mkubwa, mama Tereza tuombee tuwe na umoja.
Ulisema kama hatuwezi kulisha maelfu tumlishe mhitaji mmoja, mama Tereza tuombee tuwakumbuke wahitaji wetu.
Ulisema amani inaanza na tabasamu, mama Tereza tuombee kuishi tabasamu hilo hata tunapopitia magumu katika maisha yetu.
Ulisema furaha ni sala na ni nguvu, mama Tereza tuombee tupende kusali tupende kusali kwa furaha.
Ulisema tueneze upendo kila mahali tunapoenda, mama Tereza tuombee tueneze upendo tueneze
upendo kila tunapoenda.
Ulisema kama tunahukumu watu wengine, kama tunahukumu watu hatuna nafasi ya kuwapenda, mama Tereza tuombee tusiwe watu wa kuwahukumu wengine.