Mtunzi: Alfred Ogombo
> Mfahamu Zaidi Alfred Ogombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alfred Ogombo
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Shukrani
Umepakiwa na: Alfred Ogombo
Umepakuliwa mara 586 | Umetazamwa mara 2,476
Download Nota Download Midi1.Ninayo furaha, ninapomwimbia Yeye Bwana Mungu wangu
Nitamsifu Bwana nitamtukuza Bwana
Bwana kaniepusha nayo majanga 'kanipa afya njema
Nitamsifu Bwana nitamtukuza Bwana
Daima nitamtumikia Mungu nitaimba milele utukufu wa Bwana sifaze ntatukuza x2
2.Bwana kanilinda, Bwana siku zote hunitendea makuu –
Hivyo sinabudi mimi kumshukuru Mfalme Bwana Mtawala –
3.Sote tutambue, Bwana ni mkuu hakuna Mungu kama Yeye –
Mbinguni duniani hakuna anayelinganishwa na Mungu –
4.Bwana astahili, kusifiwa na kutukuzwa milele yote –
Jina lake takatifu na tukufu nalo lihimidiwe –
5.Bwana wa mabwana, Mungu wa miungu ndizo sifa zake Bwana –
Mungu wa Ibrahimu Mungu wa Isaka Mungu wa Yakobo –